September 27, 2016

RC MAKONDA AKAMILISHA MAANDALIZI YA KAMPENI YA 'MTI WANGU'Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo amefanya ziara katika barabara ya Airport na Barack Obama ikiwa ni maandalizi ya kampeni ya ‘Mti Wangu’ inayotarajiwa kuzinduliwa Oktoba Mosi .

Makonda amesema miti itakayopandwa Oktoba Mosi, itamwagiliwa na maji ya bomba ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (Dawasco) badala ya kutegemea mvua pekee.

"Kila mwananchi anatakiwa kuhakikisha anapanda mti na kuusimamia ukue ndipo tutaweza kufikia lengo letu la kupanda miti 4 millioni, wamiliki wa viwanda wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kwani viwanda ndivyo vinaongoza katika uchafuzi wa mazingira,"alisema Makonda.

Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema alisema:"Baada ya kupanda miti hiyo katika eneo la Airport utafuata mkakati wa kuweka mawasiliano ya intaneti bure katika vituo vya karibu ili mtu anapokuwa maeneo hayo apate huduma ya mtandao" alisema