September 27, 2016

PROF. LIPUMBA ATIMULIWA CUFMkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF)umekutana leo Zanzibar kujadili mustakabali wa nafasi ya uongozi wa Chama hicho baada ya Prof. Lipumba kurudi na kusema yeye ndo mwenyekiti halali wa Chama hicho.

Licha ya Prof.Lipumba kusema yeye ndo Mwenyekiti halali wa Chama hicho ,hajahudhuria mkutano huo kwa sababu hakupewa taarifa.Alipoulizwa kama anafahamu kuhusu kuwepo kwa mkutano huo alisema hafahamu lolote.

Baraza Kuu la Uongozi Taifa la CUF kwa kutumia uwezo wake kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Ibara ya 10 (1) (c) limemfukuza uanachama Prof . Ibrahim Lipumba. Wajumbe 42 waliohudhuria wote wamepiga kura na kuridhia kufukuzwa Prof. Lipumba. Wajumbe wote wa Baraza Kuu ni 58.