September 27, 2016

NDEGE YA PILI YA ATCL YATUA JNIANdege ya pili ya ATCL imetua JNIA mchana huu,majira ya 0953 UTC(1253 Local Time) ndege hiyo imetuwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere.Baada ya kutua,itaenda eneo la Terminal One,na baadae kuhifadhiwa eneo la JWTZ kikosi cha anga.

Ndege hii inakamilisha ujio rasmi wa ndege ya mbili zilizonunuliwa na TGFA na kukodishwa na ATCL. Kama ilivyo utamaduni wa Usafiri wa Anga, ndege hiyo yenye usajili wa C-FHNF itapata "WATER CANNON SALUTATION" na baadae kukabidhiwa kwa maafisa wa serikali.