September 27, 2016

MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR ASEMA MAFIA NI SEHEMU YA ZANZIBARKatika kikao cha Baraza la Wawakilishi leo asubuhi, Mwanasheria mkuu wa Zanzibar ameweka bayana na kuwataka wawakilishi kwenda kifua mbele na kuitetea mipaka ya nchi yao kwa hoja ambayo imo hata kwenye Katiba na maandishi mbalimbali rasmi.

Mwanasheria alifafanua kuwa tokea mwaka 1888 kisiwa cha Latham Island,Mafia na Lamu ni sehemu ya Zanzibar.

Mwaka 1890 bendera ya Sultan wa Zanzibar ilianza kupepea rasmi kisiwa cha Latham kinachogombaniwa na bara kwa sababu ya utajiri wa mafuta na gesi.

Alisisitiza kuwa tokea tarehe hiyo hakuna mtu kutoka bara au kokote duniani aliohoji umuliki wa kisiwa hicho au aliedai kuwa kisiwa hicho ni mali ya Tanganyika.