August 26, 2016

SAMATTA AFUNGA NA KUSAIDIA KLABU YAKE GENK KUFUZU EUROPA LEAGUEMchezaji wa kitamataifa kutoka Tanzania Mbwana Ally Samatta amepata nafasi ya kucheza hatua ya makundi ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League. Hii ni baada ya klabu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji kupata ushindi wa jumla wa 4-2 mechi ya kufuzu hatua ya makundi dhidi ya wapinzani wao Lokomotiva Zagreb ya Croatia.

Genk walipata ushindi wa 2-0 mechi iliyochezwa Alhamisi jioni. Klabu hizo mbili zilitoka sare 2-2 mechi ya mkondo wa kwanza. Samatta alifungia klabu yake bao la kwanza dakika ya pili naye mwenzake Leon Bailey akafunga la pili muda mfupi baada ya mapumziko.