August 26, 2016

CRISTIANO RONALDO ACHUKUA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA WA ULAYACristiano Ronaldo amewashinda wachezaji Antoine Griezman na Gareth Bale na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya kwa upande wa wanaume. Ushindi huu umetokana na mafanikio yake msimu uliokwisha huku akiwa ametwaavikombe vikubwa vya ulaya kwa maana klabu bingwa ulaya na kombe la mataifa ya Ulaya.

Ronaldo pia alikuwa mfungaji bora wa Ulaya huku akiwa wa pili kwa ufungaji katika ligi kuu ya nchini Hispania. Ikumbukwe pia, Ronaldo alifika fainali hizi huku mpinzani wake akiwa ni Antoine Griezman na kumshinda kote ijapokuwa kwenye fainali ambayo Ureno walitwaa ubingwa aliumia mapema sana.

Ronaldo alifunga mabao 51 kwenye mechi 48 msimu uliopita huku akifunga mabao 3 pekee kwenye mashindano ya mataifa ya Ulaya ambapo mchezaji Antoine Griezman alikuwa mfungaji bora.