July 4, 2016

WAZIRI MKUU AMUUNGA MKONO MAKONDA, APIGA MARUFUKU MATUMIZI YA SHISHA NCHINIWaziri mkuu Kassim Majaliwa amepiga marufuku matumizi ya shisha na kulitaka Jeshi la Polisi kufuatilia kutokomeza matumizi hayo ili kuwaokoa vijana.
Ameongeza kusema kuwa shisha ni aina ya tumbaku inayokuwa na ina mchanganyiko wa vilevi mbalimbali kama gongo na viroba na mtumiaji anapotumia kilevi hicho hukosa nguvu na hutaka kutumia kila siku na kufuata popote.