July 30, 2016

MKUU WA MKOA DODOMA ASITISHA KUHAMIA MKOANI HUMO KWA SIKU 14Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana amezitaka wizara na taasisi za Serikali kusubiri kwa siku 14 ili utolewe kwanza utaratibu wa jinsi ya kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kuhamia mjini Dodoma. 

Mbali ya Rugimbana kuzuia wizara na taasisi zake kuanza kuhamia katika mji huo ambao ni makao makuu ya Serikali, pia amepiga marufuku uuzaji wa viwanja kusubiri utaratibu huo unaofanyiwa kazi na kikosi kazi kilichoundwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Julai 26, mwaka huu. 

Chanzo: Mwananchi