July 4, 2016

AJALI MBAYA YA BASI, WATU 24 WAFARIKIAjali mbaya sana imetokea maeneo ya Maweni kati ya Dodoma na Manyoni . Basi moja lilikuwa linatokea Dar kwenda Kahama na lingine lilikuwa litatokea Kahama kuelekea Dar. 


Kamanda wa polisi mkoa singida Thobias Sedoyoka amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba ajali hiyo inahusisha basi lenye usajili wa no T 531 BCE likitokea dar kwenda kahama na basi T 247 linalotoka kahama kwenda Dar yote ya kampuni moja CITY BOYS, yamegongana uso kwa uso na kuawa abiri 24 papo hapo na kujeruhi wengi idadi zaidi ya vifo itaendelea kutolewa.