June 25, 2016

Kamishna wa UK kuhusu EU kujiuzulu

Lord Hill


Kamishna anayeiwakilisha Uingereza katika muungano wa Ulaya Lord Hill anatarajiwa kujiuzulu akisema kuwa kile kilichofanyika hakiwezi kurudishwa baada ya Uingereza kupiga kura ya kujiondoa katika muungano huo.

Katika taarifa ,amesema kuwa haamini ni sawa kwa yeye kuendelea na kazi yake kama kamishna anayesimamia huduma za fedha.Lakini ataendelea kuhudumu kwa wiki kadhaa ili ajiuzulu kwa mpangilio.

Akiwa mwandani wa waziri mkuu David Cameron ,Lord Hill amehoji kwa Uingereza kusalia katika muungano wa Ulaya.

Tangazo hilo la Lord Hill linajiri huku waziri wa kwanza wa Uskochi Nicola Sturgeon akisema kuwa ataanzisha mazungumza ya haraka na muungano wa Ulaya ili kuilinda haki ya Uskochi katika muungano huo baada ya Uingereza kujiondoa.

Chanzo: BBC