June 22, 2016

Barua za babake Obama zafichuliwaAkiwa bado kijana nchini Kenya mwaka 1958, babake rais wa Marekani Barack Obama, Barack Hussein Obama, alituma barua kwa taasisi kadha nchini Marekani akiomba nafasi ya kutimiza ndoto yake ya kusoma nchini Marekani.

Alifanikiwa kupata nafasi akaelekea chuo cha Hawaii, ambapo alikutana na mamake rais Obama, Ann Dunham ambapo mtoto wao Rais Obama alizaliwa mwaka 1961.

Barua alizoandika kutoka mwaka 1958 hadi mwaka 1964 wakati alirejea nchini Kenya, zilipatikana katika kumbukumbu katika kituo cha Schomburg eneo la Harlem mjini New York mwaka 2013 lakini ni wiki hii tu barua hizo zimefichuliwa.