May 29, 2016

WANAFUNZI WA STASHAHDA YA UALIMU MASOMO YA SAYANSI, HESABU NA TEKNOLOJIA UDOM WARUDISHWA NYUMBANIImetokea sintofahamu kwa wanafunzi wa special diploma (Education) baada ya kuambiwa chuo kimefungwa kwa upande wao hadi hapo watakapotangaziwa mustakabali wao. 

Hii ilianza pale ambapo wanafunzi hao walipoanza kudai haki yao ya kufundishwa baada ya kutoona mwalimu yeyote akiingia darasani kwa takribani wiki tatu sasa. 

Mpaka sasa haijafahamika tatizo ni nini huku tetesi zikizagaa kuwa wizara ina mpango wa kufutilia mbali aina hiyo ya elimu huku wengine wakidai walimu hawajalipwa pesa zao.