May 23, 2016

VAN GAAL AFUKUZWA MAN UTDSasa ni rasmi, Manchester United wamemfukuza kazi kocha wao, Louis van Gaal, siku mbili tu tangu alipowapatia Kombe la FA kwenye fainali iliyopigwa dhidi ya Crystal Palace dimbani Wembley. Van Gaal anaondoka na wasaidizi wake wote wa Kidachi kwenye benchi la ufundi, Albert Stuivenberg, Frans Hoek na Max Reckers ambapo Jose Mourinho ataichukua nafasi hiyo.

Ikumbukwe kwamba Mourinho alikuwa msaidizi wa Van Gaal klabuni Barcelona. Kocha huyo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Uholanzi, Bayern Munich, Bercelona, Ajax na Az anaondoka kwa sababu uongozi na wamiliki wa Man United hawaridhiki na aina ya ufundishaji wake na timu kumaliza katika nafasi ya tano kwenye Ligi Kuu ya England.