May 23, 2016

SPIKA ASEMA BAADHI YA WABUNGE HUVUTA BANGI NA UNGA, ASEMA VIFAA MAALUM KUFUNGWA KUWABAINISpika wa Bunge Job ndugai amefichua siri hiyo, Spika Ndugai amesema wanafikiria kuweka vifaa maalum vya kupima ulevi kwa watunga sheria hawa.
Spika wa Bunge amesema wanajaribu kuwatambua baadhi ya wabunge hao na kuwapa msaada wa kisaikolojia.

Maneno ya Spika; "Tunajaribu ku-identify(kuwatambua) watu maalum wanaoweza kutusaidia kuzungumza na hawa watu iliwaondokane na matatizo yale ambayo tutaweza kuyagundua... lakini wale wanaofanya kwa kificho itakuwa tabu kidogo. Lakini huko mbele tutakwenda kwenye vifaa" alisema Ndugai na kuongeza:

"Maana siyo ulevi tu, kuna sigara kubwa (Bangi), unga (Dawa za Kulevya).... watu wanapiga konyagi hadi mchana, kimsingi mambo ni mengi", alisema Ndugai.
Hata hivyo alisisitiza asieleweke vibaya sio wabunge wote hutumia vilevi wakiwa bungeni bali ni wachache.

"Simaanishi wote (Wabunge), maana mtu anaweza kufikiri ni wabunge wote... hapana. Hili ni kundi dogo mno la wabunge (na) hawajai hata mkononi. Lakini Wabunge walio wengi ni wazuru sana, hawanywi pombe wala nini. Kikundi hichi kinahitaji msaada wa ushauri" alisema.