May 1, 2016

SIMBA SC NA AZAM FC ZATOSHANA NGUVU
Simba SC na Azam FC leo wameshindwa kuwasogelea vinara wa ligi kuu ya vodacom Yanga SC baada ya kutoka sare katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo ambao Simba SC walikuwa wenyeji wa Azam FC ulimalizika kwa sare ya bila kufungana huku kila timu ikipoteza nafasi kadhaa za kujipatia magoli.

Kwa matokeo hayo Yanga wamejikita kileleni katika msimamo wa ligi wakiwa na pointi 65 na wakifuatiwa na Azam FC wenye pointi 59 na hivyo kuwa na tofauti ya pointi 6.