May 29, 2016

SERIKALI YARASIMISHA SHERIA YA UFANYAJI USAFI KILA JUMAMOSI YA MWISHO WA MWEZISerikali imerasimisha jumamosi ya kila mwisho wa mwezi kuwa ni siku ya usafi kitaifa kupitia sheria ya mazingira ya mwaka 2004 kifungu 191.

Mtu yeyote atakayekaidi kufanya usafi siku hiyo atatozwa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini au kifungo cha kuanzia miezi mitatu mpaka miaka saba.

Atakayebainika kutupa taka hovyo atatozwa shilingi laki mbili papo hapo na kwa kampuni au taasisi italipa milioni tano na kuendelea.