May 4, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AMTEUA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO KUWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Dkt. Asha-Rose Migiro anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kalaghe ambaye amerudishwa nyumbani.

Dkt. Asha-Rose Migiro ataapishwa kesho Alhamisi tarehe 05 Mei, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
04 Mei, 2016