May 1, 2016

NEEMA KWA WAFANYAKAZI: RAIS MAGUFULI ASHUSHA KODI YA MSHAHARARais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye sherehe ya Mei mosi ametoa neema kwa wafanyazi kwa kupunguza kodi ya mapato PAYE kutoka asilimia 11 mpaka asilimia 9 yaani single digit kama ilivyombwa na wafanyakazi kuptia risala iliyosomwa na Katibu Mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi ndugu Nicholaus Mgaya , 

Pia katika sherehe hizo za mei mosi, Mheshimiwa Rais amezungumzia suala la watumishi hewa. Ameeleza kwamba idadi wa watumishi hewa nchini  imeendelea kuongezeka ambapo takwimu za jana zinaonyesha kuwepo kwa watumishi hewa 10,295

Akizungumzia suala hilo, Rais  wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania  Dr John Pombe Magufuli amesema kati ya watumishi hao hewa, 8,373  wanatoka  Tamisemi   na watumishi 1.922 wanatoka serikali kuu.

Amesema watumishi hao walikuwa wakiligharimu taifa sh. Bilioni 11.6 kwa mwezi sawa na Bilioni 139  kwa  mwaka.