May 27, 2016

MBUNGE: JIMBONI KWANGU WATU WANAOGOPA KUOA WANAWAKE WAZURI
Innocent Bashungwa (CCM) wakati alipokuwa akichangia hotuba ya Wizara ya Maliasili na Utalii alisema watu jimboni kwake wanaogopa kuoa wanawake wazuri kwa sababu wanachukuliwa na wanajeshi.

'Jimboni kwangu watu hawaoi wanawake wazuri’, alisema mbunge huyo wa Karagwe,

Bashungwa wakati akichangia hotuba hiyo ameiomba Serikali kuhakikisha inaimarisha ulinzi kwenye kata ya Bweranyangi ambako wanajeshi wengi hulinda mpaka wa nchi.