May 21, 2016

'GROUP ADMINS' WA WASAP WATAHADHARISHWAMeneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), ndugu Innocent Mungi amesikika katika mahojiano na kituo cha redio cha Clouds Fm akitoa ushauri kwa wasimamizi wa makundi (group admins) wa mtandao wa WhatsApp kuwasimamia vyema wanachama wao ili kuepuka kufanya makosa ya kimtandao.

''Groups admins wawajibike na kitu tunakiita 'moderation' na wasumbufu wakemewe na ikilazimika wapigwe 'ban' '', alisema Innocent Mungi akiwa anajibu swali alilioulizwa na mtangazaji wa redio hiyo kuhusu mtu kupokea video bila ridhaa yake na kutolea mfano wanachama waliomo kwenye 'magrupu' ya WhatsApp.

Akitilia mkazo kauli yake, Mungi alinukuliwa pia akisema waendeshaji wa makundi ya WhatsApp wanaweza kuwajibika endapo watabainika kulea wahalifu wa kimtandao kwa kushindwa kuwachukulia hatua kwa utaratibu alioueleza hapo juu.