May 23, 2016

BARCELONA YATWAA KOMBE LA MFALME


Klabu ya soka ya Barcelona imetwaa kombe la Mfalme Hispania, maarufu kama Copa del Rey katika Fainali ya 114.

Wachezaji Jordi Abba na Neymar ndio walio iwezesha Barcelona kutwaa taji hilo katika Fainali iliyopigwa Jijini Madrid kwenye Uwanja wa Atletico Madrid wa Estadio Vicente Calderon.

Hii ni Fainali ya 37 ya kombe hili kwa Barcelona huku Barca wakishinda mara ya 28 sasa. Ikumbukwe Mwaka Jana, Barca walitwaa Kombe hili kwa kuifunga Athletic Bilbao 3-1.