April 9, 2016

SENDEKA: LOWASSA ANAWADANGANYA WATANZANIA

 
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema, Rais Dk. John Magufuli hatafuti umaarufu, isipokuwa anachapa kazi ili kuwaetea maendeleo Watanzania. 
 
Hayo yamesemwa na Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa tuhuma za ufuisadi, Edward Lowassa, kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa ikiwemo hali ya kisiasa nchini, kuachisha kazi watumishi wenye tuhuma mbalimbali na kile alichokiita tatizo la mfumo wa nchini, aliyosema katika mazungumzo yake na wanazuoni kutoka vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi, Aprili 7, 2016. 
 
"Alichokifanya Ndugu Lowassa ni kutaka kuwaaminisha Watanzania masuala yasiyo sahihi kwa maslahi ya kisiasa, kwani ukweli ni kwamba; Mosi Rais John Magufuli hatafuti umaarufu, badala yake yeye na Serikali yake wanachapa kazi ili kuwaletea maendeleo Watanzania kwa jumla" alisema Sendeka na kuoneza; 
 
"Pili, kuhusu suala la mfumo, Tanzania haina tatizo la kimfumo, kwani iliyopo ambayo iliwekwa na waasisi wa taifa hilo, Hayati Mwalimu Nyerere na Abeid Aman Karume ni imara na imkuwa ikiboreshwa kulingana na majitaji