April 16, 2016

RAIS MAGUFULI AMFUTA KAZI MHARIRI WA MAGAZETI YA SERIKALI
Rais wa Tanzania John Magufuli ametengua uteuzi wa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Bw Gabriel Nderumaki.

Bi Tuma Abdallah, ambaye amekuwa mhariri mtendaji msaidizi wa magazeti ya serikali (TSN), ameteuliwa kuwa kaimu.

Hakuna maelezo yoyote zaidi yaliyotolewa kuhusu sababu za kutenguliwa kwa uteuzi wa Bw Nderumaki.

TSN huchapisha magazeti ya Daily News, Sunday News, habari Leo, Habari Leo Jumapili na Spoti Leo.

Chanzo: BBC

Soma hapo chini Taarifa ya Ikulu 

TAARIFA YA IKULU KWA VYOMBO VYA HABARI 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Bw. Gabriel Nderumaki.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 14 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia tarehe 18 Machi, 2016.

Kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Bi. Tuma Abdallah kukaimu nafasi hiyo.

Bi. Tuma Abdallah ni Mhariri Mtendaji Msaidizi wa Magazeti ya Serikali (TSN)

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
14 Aprili, 2016