April 15, 2016

OMBA OMBA NA WAPIGA DEBE WAANZA KUPATA MISUKOSUKO DARAgizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda limeanza kufanyiwa kazi baada ya karandinga kuanza kuwasomba ombaomba waliojaa katika maeneo mengi jijini hapa.

Makonda alitangaza kuanza kuwaondoa ombaomba hao juzi, huku akipiga marufuku wananchi kuwapa pesa kwa kuwa ndicho chanzo cha kuwapo kwao jijini hapa.

‘Mchakamchaka’ wa kuwaondoa watu hao ulianza juzi usiku katika maeneo ya Mnazi Mmoja, Samora na Kariakoo. 

Makonda alisema ikifika Jumatatu kama hawajajisalimisha Serikali itachukua hatua kali na kuwarudishwa walikotoka. “Kwanza ni kinyume cha sheria, pili ni hatari kwa maisha yao na watoto wanatakiwa warudi shule sasa,” alisema.

Kadhalika, operesheni hiyo licha ya timuatimua kuwakumba ombaomba, wapigadebe nao wameunganishwa katika kundi hilo kwa kuanza kuondolewa kwenye vituo vya mabasi.