April 7, 2016

MWANA WA BESIGYE ASHINDA URAIS OXFORDMtoto wa mwanasiasa machachari nchino Uganda Dr.Kizza Besigye anayemnyima usingizi Rais Museveni ameshinda nafasi aliyokuwa anagombea katika Chuo kikuu cha Oxford nchini Uingereza
Mtoto huyo wa kiume aitwae Anslem Besigye aliwagaragaza washindani wake na kutwaa nafasi ya urais wa mijadala (debate) katika bweni lake Anslem Besigye alikuwa ametengeneza video fupi ya kuomba wanafunzi wenzake wampigie kura.

Mamake Winnie Byanyima amefurahia ushindi wa mwanawe na kuandika kwenye Twitter: “Ameshinda! Anslem amechaguliwa rais wa chama cha mijadala katika bewa lake. Najionea fahari kama mamake.”

Kwenye video aliyokuwa ameitengeneza alikuwa amesimulia mambo ambayo amefanyia chama hicho na uzoefu wake katika mijadala.Mwisho wa video mamake Bi Byanyima, alionekana na kusema “huna budi kushinda uchaguzi huu, nimekusaidia sana!”.

Babake Anslem, Dkt Kizza Besigye, amewania urais mara nne dhidi ya kiongozi wa muda mrefu wa Uganda Yoweri Museveni bila mafanikio.

Chanzo: BBC