April 9, 2016

MSANII NDANDA KOSOVO AFARIKI DUNIAMwanamuziki‬ nguli wa Muziki wa Dansi nchini Tanzania "Ndanda Kosovo" amefariki Dunia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Taarifa za awali zinasema marehemu alifikishwa hospitalini hapo kupata matibabu ya Vidonda vya tumbo vilivyokuwa vikimsumbua siku chache zilizopita lakini alifariki mapema asubuhi ya leo.

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina.