March 11, 2016

YANGA YATUA RWANDA, NI GUMZO.

 
Kikosi cha Yanga kilipokuwa kwenye pipa kuelekea Rwanda


WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika Yanga, jana waliwasili Kigali, Rwanda na kutamba kuibuka na ushindi dhidi ya APR katika mchezo utakaofanyika kesho.Ujio wa Yanga iliyowasili asubuhi, umekuwa gumzo katika Jiji la Kigali kutokana na mabingwa hao wa Tanzania kuonekana kuwa tishio katika Ukanda wa Afrika Mashariki. Mashabiki wamekuwa wakiizungumzia mno mechi hiyo, hasa `uzito’ wa Yanga yenye nyota waliowahi kuichezea APR, Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite. 

Aidha, mara baada ya kikosi cha Yanga kutua kwa ndege kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Kanombe uliopo kilometa chache kutoka Uwanja wa Amahoro, eneo la Kicukiro jijini Kigali, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm aliwaambia waandishi wa habari kuwa, ushindi ndio uliowapeleka nchini humo. 

“Tunataka kushinda na hicho ndicho kilichotuleta. Lakini tunajua APR ni timu nzuri, tunaheshimu hilo. Lakini hakika tunataka kutengeneza mazingira bora ya mechi ya marudiano kule Dar es Salaam.