March 8, 2016

YANGA YAITANDIKA AFRICAN SPORTS NA KUREJEA KILELENIKlabu ya Yanga leo Machi 8.2016 wamefanikiwa kurejea kileleni mwa ligi Kuu ya soka ya Tanzania Bara (VodaCom Premier Legue-VPL) kwa kuiangushia kipigo cha mabao 5-0 African Sports kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. 

Wafungaji wa Yanga ni pamoja na Kelvin Yondani, Ngoma, Tambwe na  Matheo. Mchezo huo wa aina yake, Yanga ilijihakikishia ushindi mapema baada ya kupata mabao kuanzia kipindi cha kwanza tu cha mchezo na hadi kufikia kipindi cha pili walikwisha jifikishia mabao 5-0. 

Kwa ushindi huo, Yanga inarejea tena kileleni mwa ligi huku kwa kufikisha pointi 50 na kuwashusha watani zao Simba SC ambao walikuwa wanaongoza ligi hapo awali ambao sasa wamerudi hadi nafasi ya pili kwa kubakia na pointi zao 48 za awali, huku Azam wao wakibakia nafasi hiyo hiyo ya tatu kwa kuwa na pointi 47.