March 10, 2016

WAZIRI WA ELIMU NDALICHAKO LEO ATUA CHUO CHA MT JOSEPH DAR


Chuo Kikuu cha Mt. Joseph kimechukua vichwa vya habari hivi karibuni baada ya kutokea kwa migomo kwenye vyuo vishiriki vya chuo hicho na baadhi kufutiwa vibali vilivyoanzisha vyuo vikuu viwili vishiriki vya Mt Joseph ambavyo ni chuo kikuu kishiriki cha sayansi ya kilimo na Teknolojia ‘SJUCAST’-Arusha na chuo kikuu kishiriki cha teknolojia ya Habari Mawasiliano ‘SJUIT’-Songea. 

Chuo cha Mt Joseph nao waligoma kuanzia mwanzoni mwa juma hili wakiwa na madai mbalimbali ikiwemo kufundishwa mtaala ambao haupo nchini pamoja na wakufunzi wasio na sifa. Leo March 9 Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amefika chuoni hapo na kutoa maelezo ikiwa ni juhudi za kutatua mzozo huo.