March 8, 2016

TUNAWATAKIA MAADHIMISHO MEMA YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Leo tarehe 8 Machi ya kila mwaka Tanzania huungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. 

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake, hutoa fursa kwa Serikali, wananchi, wadau, na wanawake wenyewe kupima utekelezaji wa maazimio, matamko na mikataba ya Kimataifa, Kikanda na Kitaifa inayohusu masuala ya maendeleo ya wanawake na usawa wa jinsia. 

Siku ya wanawake Duniani husisitiza kujenga mshikamano wa wanawake wote duniani, kuhamasisha jamii kutafakari kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake ya kila mwaka; kuelimisha jamii kuhusu jitihada mbalimbali zilizofanywa na Serikali na asasi mbalimbali yakiwemo Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kuwaendeleza wanawake; na kuhamasisha jamii kuhusu utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali ya Serikali yenye lengo la kudumisha Amani, Usawa na Maendeleo.

"MAKAMBAKO KWETU INAWATAKIA KILA LA KHERI WANAWAKE WOTE DUNIANI"