March 10, 2016

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SEKRETARIETI YA AJIRA, MACHI 2016


TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
 Kumb. Na EA.7/96/01/I/02 
09 Machi, 2016
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Ministries, Departments and Agencies and Local Government Authorities (MDA’s & LGA’s), National College of Tourism (NCT), Institute of Judicial Administration Lushoto (IJA), Tanzania Public Service College (TPSC), National Food Reserves Authority (NFRA) na Weight and Measures Agency (WMA), anatarajia kuendesha Usaili na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili.

Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia yafuatayo:
1. Usaili utaanza saa moja kamili asubuhi (1:00) na utafanyika mahali na tarehe kama inavyoonesha katika nafasi husika.
2. Kuja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho cha mkazi, kupigia kura, kazi, hati ya kusafiria n.k
3. Kuja na Vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne, sita, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji na mahitaji ya sifa kwa kada husika..
4. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
6. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
7. Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanyia usaili.
8. Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)
9. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU & NECTA)
10. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo, hivyo wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa.

KUFUNGUA TANGAZO KAMILI NA ORODHA YA MAJINA(PDF) BOFYA HAPA