March 16, 2016

TANGAZO LA KUITWA KAZINI SEKRETARIETI YA AJIRA MACHI 16,2016
TANGAZO LA KUITWA KAZINI

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe 10/02/2016 hadi tarehe 23/02/2016 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi umekamilishwa.

Orodha ya majina ya waliopangiwa vituo vya kazi ni kama yanavyoonekana katika Tangazo hili. Katika Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Data base) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi za kazi kupatikana.

Aidha, wanatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa katika muda ambao umeainishwa kwenye barua zao za kupangiwa vituo vya kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira.

Barua za kuwapangia vituo vya kazi zimetumwa kupitia anuani zao za posta. Kwa wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.

KUFUNGUA TANGAZO (Pdf) BOFYA HAPA