March 10, 2016

TANGAZO LA KUITWA KAZINI SEKRETARIETI YA AJIRA MACHI, 2016


TANGAZO LA KUITWA KAZINI

Kumb. Na. EA.7/96/01/I/5 
10 Machi, 2016

 Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwa taarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe 10/02/2016 hadi tarehe 23/02/2016 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi umekamilika.

Orodha ya majina ya waliopangiwa vituo vya kazi ni kama yanavyoonekana katika Tangazo hili. Katika orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

Aidha, wanatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa katika muda ambao umeainishwa kwenye barua zao za kupangiwa vituo vya kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na Mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira. Barua za kuwapangia vituo vya kazi zimetumwa kupitia anuani zao za posta.

Kwa wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.

NB: Kwa wale waliopangiwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wanatakiwa kuripoti Chuo cha Utalii Tandika tarehe 21 Machi, 2016 saa mbili kamili asubuhi bila kukosa kwa ajili ya maelekezo na taratibu nyingine.

KUFUNGUA ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KAZINI(PDF) BOFYA HAPA