March 23, 2016

SERIKALI YAIPIGA MARUFUKU BODI YA NHC KURUHUSU UJENZI WA MIRADI MIPYA YA KIBIASHARAWaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amepiga marufuku bodi ya shirika la Nyumba la Taifa kuruhusu ujenzi wa miradi mipya ya kibiashara. Sambamba na hilo Waziri Lukuvi amepiga marufuku Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupandisha kodi kwa nyumba za Serikali bila kumhusisha.

Aidha Waziri Lukuvi ameitaka NHC kujenga nyumba za bei nafuu kwa kuwa zilizopo sasa ni ghali kwa watanzania walio wengi, hivyo kushindwa kumudu gharama hizo.Maagizo hayo ameyatoa wakati akizungumza na bodi ya NHC Jijini Dar es Salaam.