March 8, 2016

NSSF YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUFANYA USAFI NA KUTOA MSAADAKatika kuadhimisha siku ya Mwanamke Duniani Shirika la Hifadhi ya Taifa la NSSF Mkoa wa Lindi kwa Kushirikiana na Wanawakewa Manispaa ya Lindi kwa kufanya Usafi na kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo sabuni za Kuogea na Kufulia kwa akina mama wajawazito na wale waliojifungua ambao wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Sokoine Mjini Lindi ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani. 

Akizungumza kwenye hafla hiyo ya kutoa msaada huo,Meneja wa NSSF mkoa wa Lindi Bi Nour Aziz amesema Shirika lake limechukua hatua hiyo kuadhimisha siku ya wanawake duniani Huku akitoa wito kwa wakazi wa Mji Huo Kunufaika na Mafao ya Matibabu yanayotolewa na Nssf

“Leo ni siku ya wanawake duniani kote,NSSF kwa Kutambua Umuhimu wa wanawake imeona ni vyema iwashukuru wananchi wa Lindi Hususan wanawake kwa Kuamua Kushiriki katika Usafi na Utoaji wa Misaada kwa Wagonjwa” 

Sambamba na Maadhimisho hayo Bi Nour Aziz amebainisha Kuwa shirika lake Linatoa pia mafao ya Uzazi ambapo Mafao hayo hulipwa kwa wanachama wanawake wanaotegemea kujifungua au wameshajifungua.

Pia Meneja Huyo ameeleza kuwa sifa zinazotakiwa ili unufaike na Fao ni pamoja na kuchangia angalau michango 36 kati ya hiyo michango 12 iwe imefanywa karibu na wiki ya kujifungua Au anaetegemea kujifungua au ameshajifungua motto na ulipwa kila baada ya miaka mitatu isipokuwa ikiwa mtoto atafariki ndani ya miezi 12 baada ya kuzaliwa na Madai yafanyike kabla ya kujifungua au ndani ya siku 90 baada ya kujifungua 

Pamoja na Fao hilo pia NSSF hutoa Matibabu kwa magonjwa yanayoambatana na ujauzito wa mwanachama baada ya wiki ya 24 ya ujauzito na huishia masaa 48 baada ya kujifungua au siku 7 ikiwa kajifungua kwa upasuaji na Matibabu haya hufanywa katika hospitali ambazo zimeingia mkataba na Shirika wa kutibu wanachama wa NSSF

Katika katika Kuadhimisha Siku Hiyo wafanyakazi wanawake wa NSSF Lindi waliungana na wanawake wengine Katika Kuhakikisha Hospital hiyo Inakuwa safi.