March 21, 2016

MSAFARA WA KAMATI YA BUNGE YA TAMISEMI WAPATA AJALIMsafara wa Kamati ya Bunge ya TAMISEMI uliokuwa unaongozwa na gari ya polisi ambayo ilikuwa ina alert approaching vehicles kuwa kuna msafara umepata ajali.Kwenye eneo la mlima polisi walikutana na Toyota spacio ikiwa speed sana wakamu-alert juu ya kuwepo msafara mbele lakini akagoma na kuendelea,ghafla akakutana na msafara na kusimama ghafla kitendo kilicho sababisha Lori liigonge spacio na kuhama na kwenda kuparamia magari 3 ya msafara.

Majeruhi sita wamekimbizwa muhimbili hali zao sio nzuri sana kwani wamepoteza damu nyingi,kwa upande wa marehemu Wamefariki watano; DPLO Hilda, Mwanasheria Kiliba na Pallangyo Mchumi, madereva wawili; mmoja gari la TASAF mwigine gari ya Mkurugenzi. 

Walioumia ni DED Matovu, Juliana -- Engineer wa maji, mweka Hazina Mashauri , Mwangata - Afisa Maendeleo ya Jamii na Amadeus Mbuta Mratibu TASAF.