March 11, 2016

MKUU WA WILAYA AAGIZA WALIMU KUJIHIMU KUFAGIA SHULENIDC Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza amewaagiza walimu wote kufanya usafi katika vituo vyao vya kazi kuanzia saa kumi na mbili na nusu asubuhi mpaka saa nne asubuhi kila Jumamosi ya kila wiki kuanzia kesho na mahudhurio yatakuwa yanachukuliwa. 

Wadau wanahoji, Mwalimu anaye amka kila siku asubuhi Jumatatu mpaka Ijumaa, bado ana kazi ngumu ya kuhangaika na watoto kwa siku hizo za kazi, Unamwambia arudi tena jumamosi saa kumi na mbili na nusu afanye usafi, atapata wapi muda wa kupumzika?