March 11, 2016

MKONGWE PAUL SCHOLES AIPONDA MANCHESTER UNITEDManchester United ilikuwa haifai na haikuwa na mpangilio wowote ilipofungwa 2-0 na Liverpool kulingana na Paul Scholes ambaye alikuwa kiungo wa kati wa timu hiyo Paul Scholes. Daniel Sturridge na Firmino walifunga bao kila mmoja na kudidimiza matumaini ya Manchester United huku David De gea akizuia mashambulio mengi ya Liverpool.

Scholes ambaye aliichezea Manchester United mara 718 aliambia BT Sport kwamba kilabu hiyo ya Old Trafford huwa na viwango fulani lakini kufikia sasa imefeli kuafikia viwango hivyo.Aliongezea:Liverpool ilikuwa na mpango wa kucheza,Lakini United hawakuwa na mpango wowote.