March 10, 2016

MBEYA WAFANYA MAOMBI MAALUM YA KUMWOMBEA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI NA SERIKALI YAKE

Picha ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ikiwa imeshikwa na maaskofu wa makanisa mbalimbali Mkoani Mbeya kwa ajili ya kufanya maombi maalumu kwa ajili ya rais na serikali yake katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya .
Muongozaji Mkuu wa Maombi ya kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli ,Askofu Dkt  Charles Gadi wa kanisa la The City of refuge Church  yenye makao makuu jijini Dar es salaam akiomba na waumini walioshiriki katika maombi hayo katika ukumbi wa Mkapa .
Baadhi ya waumini walioshiriki Maombi Maalum ya Kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake yaliyoandaliwa na Jukwaa la wakristo Mkoani Mbeya kwa kushirikiana na Askofu Mkuu wa Kanisa la The City of refuge Church Dkt Charles Gadi katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya March 8 mwaka huu.
Kwaya zikiendelea kutumbuiza katika maombi hayo ya kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya Machi 8 mwaka huu.
Baadhi ya viongozi wa makanisa mbalimbali mkoani mbeya wakiwa katika maombi maalumu ya kumwombea Rais Dkt Maguli na serikali yake .