March 16, 2016

MAN CITY HAOOO ROBO FAINALI KLABU BINGWA ULAYAKlabu ya Manchester City  usiku wa kuamkia leo wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa jumla ya mabao 3-0, baada ya mchezo wao uliopigwa katika dimba la Etihad, kumalizika kwa sare ya 0-0 dhidi ya wapinzani wao Daynamo Kyiv. 

Matokeo hayo ya sare ya bila kufungana yalitegemewa kwa hamu kubwa na mashabiki wa klabu hiyo ya Manchester City ilikuweza kusonga mbele kwenye michuano hiyo na hadi kipyenga cha mwisho matokeo yalibaki 0-0. 

Mchezo wa awali City ilifanikiwa kutoa kichapo kwa Dynamo Kyiv cha mabao 3-1, hivyo katika mchezo wao huo usikuu huu unawafanya kutinga hatua hiyo ya robo fainali kwa jumla ya pointi nne na mabao 3-1. 

Kwa upande wa mchezo mwingine kati ya Atletico Madrid na PSV hadi kipyenga cha mwisho timu hizo zilitoka sare ya 0-0. Hata hivyo kipindi cha nyongezadakika 30, pia zilitoka sare 0-0. Hata hivyo Atletico imefanikiwa kuingia hatua ya robo baada ya kupata ushindi wake kwa njia ya matuta  kwa kupaata penati 8-7 dhidi ya wapinzani wao hao