March 12, 2016

DUKA KUBWA LA FILIKUNJOMBE LAZINDULIWA

Mkurugenzi wa Mauzo wa Kampuni ya Jumbo Camera House, Mathias Luoga akionesha vifaa mbalimbali vya kamera wakati wa uzinduzi wa duka jipya lililopo Jengo la NSSF Benjamin Mkapa, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Sara Filikunjombe,  mke wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ludewa, marehemu Deo Filikunjombe ambaye pia mmiliki wa kampuni hiyo.
Mke wa marehemu Filikunjombe, Sara  (wa pili kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Prodaction, Ritta Poulsen (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Jumbo Camera House, Paul Buckendahl (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Mauzo wa Kampuni hiyo, Mathias Luoga wakigongeana glasi zenye Champagn wakati wa hafla hiyo.
Wageni waalikwa wakioneshwa moja ya kamera na vifaa vyake inayouzwa katika duka hilo kubwa la aina yake.i.
Paul akiwaongoza wageni waalikwa kusimama kwa dakika moja kumkumbuka marehemu Deo Filikunjombe.
 Mgeni rasimi katika hafla hiyo, Ritta Poulsen akihutubia wakati wa uzinduzi wa duka hilo

PICHA NA RICHARD MWAIKENDA