March 9, 2016

BAWACHA MAKAMBAKO WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUWATEMBELEA WATOTO WENYE ULEMAVU

Katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani, Baraza la Wanawake la Chadema(BAWACHA)-Makambako waliwatembelea watoto wenye ulemavu katika kituo cha Makambako. Kuwatembelea kwao kulienda sambamba na kutoa zawadi mbalimbali kwa watoto hao katika kuonyesha upendo kwao kama watu au watoto wengine.

BAWACHA Makambako wamefanya kitendo kizuri sana na kinachostahili kuigwa na jamii na makundi yote nchini  na mahali popote.


Baraza la Wanawake la Chadema wakiwa kwenye kituo cha kulelea watoto wenyenye ulemavu walipoenda kuwatembelea.
Watoto wenye ulemavu waliotembelewa na BAWACHA- Makambako siku ya maadhimisho ya Wanawake Duniani.
Baadhi ya zawadi walizoletewa watoto hao walipotembelewa na BAWACHA
Picha ya pamoja ya watoto na BAWACHA, pamoja na viongozi wengineo wa chama akiwemo Mhe. Diwani wa kata ya Makambako Bwa. Tweve na aliyekuwa mgombea wa Ubunge Bw. Mhema.