March 14, 2016

ARSENAL YATOLEWA KOMBE LA FAMichuano ya FA iliendelea tena jana kwa mabingwa wake Arsenal kuvuliwa ubingwa baada ya kuchapwa na Watford kwa mabao 2-1. Mabao ya Watford yalifungwa na Odion Ighalo na Adlene Guedioura huku bao la kufutia machozi la Arsenal likifungwa na Danny Welbeck.

Katika mchezo mwingine Manchester United wakiwa nyumbani walibanwa mbavu na West Ham united kufuatia sare ya bao 1-1. Goli la West Ham lilifungwa na mchezaji Dimitri Payet dakika ya 68 kipindi cha pili, huku bao la kusawazisha la Manchester United likipachikwa na Anthon Martial Dakika ya 83 kipindi cha pili.