February 23, 2016

LUIS SUAREZ ASAHAU PASIPOTI YAKEArsenal karibia ibahatike na zawadi ya kushangaza kutoka kwa mshambuliaji wa kilabu ya Barcelona Luis Suarez baada ya mchezaji huyo kuwacha pasipoti yake nyumbani kabla ya timu yake kuondoka kuelekea mjini London.

Haijulikani iwapo alisahau cheti hicho cha kusafiria kwa kusahau au la,lakini ni bahati mbaya kwa mashabiki wa Arsenal, mtu mmoja kutoka kilabu hiyo alitumwa kwenye nyumba ya raia huyo wa Uruguay ili kuichukua na mchezaji huyo alifanikiwa kuondoka na kikosi kizima cha Barcelona.

Mshambuliaji huyo amekuwa akifanya mazoezi tayari kwa kinyanganyiro hicho katika uwanja wa Emirates nchini Uingereza siku ya Jummanne.

Washambuliaji wa Barcelona Lionel Messi,Suarez na Neymar wamefunga mabao 91 kati yao msimu huu huku Suarez akifunga mabao 41.