January 16, 2016

TCRA YAVIFUNGIA VITUO VYA TELEVISHENI NA REDIO 24: ORODHA YOTE IKO HAPA

Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania, TCRA leo imevifungia vituo 21 vya Radio na 6 vya Television kwa muda wa miezi 3 kikiwemo kituo cha Star TV, Radio free Afrika, Kiss Fm na Uhuru FM.

Mwezi Julai 2015 ilitolewa taarifa kwa umma na TCRA kwamba baadhi ya redio na Televisheni zipatazo 40 zinadaiwa ada na tozo mbalimbali, hata hivyo Septemba 28 wakapewa onyo la mwisho kwamba hadi Tarehe 31 Disemba wawe wamelipa ada zao baadhi wakalipa na Wengine wakapuuza.

Hivyo wamefungiwa kuto kutoa huduma kwa miezi 3 na kulipa ada/kodi, TCRA wanasema hata miezi 3 ya adhabu ikiisha na bado hawajalipa, hatua zaidi zitachukuliwa.  

Sasa basi TCRA wanasema kuanzia Jumatatu tar 18, Radio 21 na TV 6, vituo hivi havitatakiwa kuwa hewani kufanya kazi kutokana na tamko la Mkurugenzi wa TCRA 

ORODHA YA VITUO VYA TELEVISHENI NA REDIO ZILIZOFUNGIWA HIZI HAPA.
1. Sibuka FM
2. Breez FM
3. Country FM
4. Ebony FM
5. Hot FM
6. Impact FM
7. Iringa Municipal TV
8. Kiss FM
9. Kitulo FM
10. Kifimbo FM
11. Mbeya City Municipal TV
12. Radio 5
13. Radio Free Afrika (RFA)
14. Musa Television Network
15. Pride FM radio
16. Radio Huruma
17. Radio Uhuru
18. Star TV
19. Rock FM Radio
20. Standard FM radio
21. Sumbawanga Municipal TV
22. Tanga City TV
23. Top Radio FM limited
24. Ulanga FM