January 29, 2016

MAWAKILI WAOMBA WANAWAKE WENYE VIRUSI VYA ZIKA WARUHUSIWE KUTOA MIMBAKundi la mawakili, wanaharakati na wanasayansi nchini Brazil limewasilisha ombi mahakama ya juu nchini humo likitaka wanawake wenye virusi vya Zika waruhusiwe kutoa mimba.

Virusi vya Zika vinaaminika kusababisha watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo, na kudumaza ubongo.

Utoaji mimba nchini Brazil hauruhusiwi kisheria, ila tu wakati wa dharura ya kiafya au iwapo mimba imetokana na ubakaji hali ambayo kwa Kiingereza inajulikana kama microcephaly. Hata hivyo mwaka 2012, uliruhusiwa kwa watu walioathiriwa na ugonjwa mwingine wa ubongo kwa jina anencephaly.

Wataalamu wameonya kwamba idadi ya watu walioambukizwa na virusi vya Zika mwaka huu huenda ikafikia kati ya milioni tatu au nne mwaka huu mabara ya Amerika. Ombi hilo mpya litawasilishwa mahakama ya juu katika kipindi cha miezi miwili.