December 6, 2015

WALIOITWA KAZINI DISEMBA 2015 NA SEKRETARIETI YA AJIRA


TANGAZO LA KUITWA KAZINI.
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe 16/11/2015 hadi tarehe 19/11/2015 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi umekamilishwa.

Orodha ya majina ya waliopangiwa vituo vya kazi ni kama yanavyoonekana katika Tangazo hili. Katika orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Data base) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

Aidha, wanatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa katika muda ambao umeainishwa kwenye barua zao za kupangiwa vituo vya kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira.

Kwa wale ambao wako karibu na Dar es Salaam na wangependa kuchukua barua zao za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya ajira kabla hazijatumwa Posta wanaruhusiwa kufanya hivyo kuanzia tarehe 7 hadi 11 Desemba, 2015. Baada ya tarehe 11 Desemba, 2015 barua zilizobaki zitatumwa kwa wahusika kwa kutumia anuani zao za posta.

Ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.

KUFUNGUA MAJINA (pdf) BONYEZA HAPA