December 6, 2015

RAIS MSTAAFU JK ATUNUKIWA TUZO UINGEREZA


Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Cheti cha heshima ya Juu ya CPTM (Companion Award). Tuzo hiyo imetolewa wakati wa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPTM ambao uliambatana na maadhimisho ya Miaka 20 ya Taasisi hiyo jijini London


Taasisi ya Commonwealth Partnership for Technological Management (CPTM) inayojishughulisha na kukuza ushirikiano katika nyanja ya sayansi na teknolojia kwa nchi za Jumuiya ya Madola, imemtunuku Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, heshima ya Juu ya CPTM (Companion Award) kwa kutambua mchango wake katika kuhamasisha ukuaji wa matumizi ya sayansi na teknolojia ikiwemo matumizi ya huduma za fedha kwa njia ya simu.