December 7, 2015

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA TPA, MWENYEKITI WA BODI NA KATIBU MKUU UCHUKUZIRais John P. Magufuli leo amevunja Bodi ya Bandari ya Jijini Dar es Salaam, kutokana na kashfa ya upotevu wa makontena ulioisababishia Serikali hasara ya mabilioni ya Shilingi. 

Mbali na kuvunja bodi hiyo, pia ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mhandisi Prof. Joseph Msambichaka na kumsimamisha kazi Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Shaaban Mwinjaka. 

Maamuzi hayo yametolewa Jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, kwa niaba ya Rais ambapo amenukuliwa akisema maamuzi hayo ya Rais yamekuja muda mfupi baada ya kubaini kasoro nyingi za kiutendaji kwa watumishi hao wa Serikali. 

Pamoja na mambo mengine, amesema Rais amewasimamisha kazi maofisa nane kutoka Bandari ya Dar es Salaam baada ya kubainika walihusika kwa namna moja ama nyingine katika sakata hilo. 

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, mara baada ya agizo hilo, ameagiza wahusika wote wakamatwe na wawekwe chini ya ulinzi ili kusaidia upelelezi ikiwa ni pamoja na kueleza makontena yaliyopotea yalikuwa ya nani na yalikuwa na thamani ya shilingi ngapi. 

Watuhumiwa hao watatakiwa kuwezesha makontena hayo yaweze kulipiwa kodi kutokana na awali kutolipiwa kodi.Katika ziara aliyoifanya katika Shirika la Reli Nchini (TRL), Waziri Mkuu alibaini matumizi mabaya ya fedha ya Sh.Bilioni 13 nje ya utaratibu ambao uchunguzi unakamilishwa kwa waliohusika.

Massawe aliteulia na Samwel Sitta kushika nafasi ya Mhandisi Madeni Kipande aliyesimamishwa kwa tuhuma za utendaji mbovu ili kupisha uchunguzi.