December 30, 2015

MBWA KUPEWA NISHANI YA USHUJAAMbwa wa polisi aliyeuawa wakati wa msako baada ya mashambulio ya Paris atatunukiwa nishani kuu ya ushujaa. Diesel, mbwa aina ya Belgian Shepherd mwenye umri wa miaka saba, alifariki wakati wa operesheni ya kumsaka mshukiwa mkuu wa mashambulio hayo.

Mbwa huyo atatunukiwa nishani kwa jina Dickin Medal ambayo hutolewa an shirika la kuwatunza wanyama la PDSA. Hadhi yake ni sawa na nishani ya Msalaba wa Victoria inayopewa watu mashujaa vitani.

Mbwa ‘shujaa wa Paris’ avuma mtandaoni
Kitambulisha mada #JeSuisChien (Mimi ni mbwa) kilivuma sana kwenye Twitter baada ya Diesel kuuawa. Diesel atapewa nishani hiyo kwenye sherehe mwaka ujao.